• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Mikel Arteta aongea kwa mara ya kwanza toka athibitike kuwa na corona

    (GMT+08:00) 2020-03-24 09:55:51

    Kocha wa klabu ya Arsenal ya England Mikel Arteta ameongea na La Sexta kwa mara ya kwanza toka athibitike kuwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID 19). Arteta mwenye miaka 37 ameongea na kueleza hali yake inaendelea vizuri na anaamini kuwa ana siku 3 hadi nne za kurejea katika hali yake ya kawaida na mwili kurejesha nguvu. Mike Arteta alibainika au kugundulika kuwa ameambukizwa virusi vya corona baada ya mchezo wa Arsenal wa Europa League dhidi ya Olympiacos. Mhispania huyo anakuwa kocha wa kwanza wa ligi ya Premier kugundulika kuwa na corona Machi 12. Awali wachezaji wa Arsenal walitakiwa kuripoti leo Jumanne mazoezini, baada ya kumaliza kujitenga kwa siku 14 kufuatia ripoti za Arteta kuwa na virusi vya corona, lakini klabu imeahirisha kutokana na hali kuwa mbaya Zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako