• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Manchester United yampigia hesabu kali Jack Grealish

    (GMT+08:00) 2020-03-24 09:56:10

    Nahodha wa kikosi cha Aston Villa, Jack Grealish amewekwa kwenye hesabu kali za kutua ndani ya Klabu ya Manchester United ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kwenye usajili ujao. Grealish anakipiga timu moja na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ambapo kikosi chake kinahaha kujinasua kutoka kwenye nafasi ya kushuka daraja. Imeelezwa kuwa United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksjaer ipo kwenye mpango wa kumpata nyota huyo ambaye amekuwa kwenye ubora wake msimu huu wa 2019/20 akitupia mabao 14.

    Aston Villa kwenye msimamo ipo nafasi ya 19 ikiwa imecheza mechi 28 imejikusanyia pointi 25 kibindoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako