• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Madaktari wa timu za Ligi Kuu England wawaonya mabosi wa timu kujiandaa na majeraha ya wachezaji

    (GMT+08:00) 2020-03-24 09:56:46

    Madaktari wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England wamewaonya mabosi wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu England kwamba wanapaswa wajiandae na kesi za wachezaji wao kuumia misuli iwapo watajaribu kumaliza ligi hiyo Juni 30. Kwa sasa mechi za Ligi Kuu England zimesimama kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea kuanza Aprili 30 huku ikitarajiwa kukamilika Juni 30. Wasiwasi wa uwepo wa Virusi hivyo unafanya ligi kufikiriwa kuwa iwapo itaanza kuchezwa Mei Mosi kutakuwa na mechi nyingi kwa timu moja jambo ambalo lina hatari kwa afya za wachezaji. Kutokana na kesi hii hakuna timu yenye njia mbadala zaidi ya kukubaliana na hali na itawalizimu kucheza mechi mbili ama tatu ndani ya wiki moja ili kukimbizana na muda huku zile zinazoshiriki michuano ya Kombe la FA watakuwa na ratiba ngumu za kukamilisha. Mmoja wa madakatari wa timu ambazo zipo nafasi ya juu amesema kuwa ni agizo kubwa kwa wachezaji kucheza Jumamosi, Jumatano na Jumamosi tena ni ratiba iliyobana na itakusanya majeruhi wengi bila mashaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako