• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kuimarisha uungaji mkono kwa nchi za Afrika katika kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-24 10:05:41

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Amesema vifaa vinavyotolewa na serikali ya China vitafikishwa Afrika kwa vipindi tofauti, China pia itahimiza makampuni ya China na mashirika binafsi yazipatie nchi za Afrika msaada. Amesema China na Afrika ni ndugu, ambao wanaungana mikono na kusaidiana siku zote. Nchi na mashirika ya kikanda ya Afrika yameiunga mkono China tangu virusi vya Corona vilipuke, na China inafuatilia hali ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika na kuzipatia msaada nchi za Afrika na Umoja wa Afrika.

    Ameongeza kuwa China imefanya mkutano kwa njia ya video na nchi za Afrika ili kuzielezea uzoefu wa China katika kupambana na virusi vya Corona, pia imetume timu za madaktari wa China barani Afrika kushiriki kwenye mapambano hayo dhidi ya virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako