• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yaunda kamati 3 dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-24 10:48:27

    Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa jana alisema serikali imeunda kamati tatu zinazoshughulikia mapambano dhidi ya janga la COVID-19.

    Bw. Majaliwa amesema kamati ya kwanza itaongozwa naye, ambayo itaundwa na baadhi ya mawaziri, makatibu wakuu na msemaji mkuu wa serikali.

    Kamati ya pili inayoundwa na makatibu wakuu wa wizara husika na itaongozwa na katibu mkuu kiongozi. Na kamati ya tatu inayoundwa na wataalamu itaongozwa na katibu mkuu wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.

    Bw. Majaliwa amesema kamati hizo tatu zitakabidhiwa jukumu la kuimarisha mapambano dhidi ya virusi vya Corona ambavyo hadi sasa watu 12 wameambukizwa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako