• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yathibitisha kesi tisa mpya za COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-24 17:38:58

    Uganda imeripoti kesi nane mpya zilizothibitishwa kuwa na virusi vya Corona (COVID-19), na kufanya jumla ya idadi za kesi hizo kufikia tisa.

    Waziri wa Afya nchini humo Ruth Aceng amesema kesi zote nane mpya ni raia wa Uganda waliowasili nchini humo wakitokea Dubai, Falme za Kiarabu kupitia ndege za Emirates na Ethiopian kati ya tarehe 20 na 22 mwezi huu. Amewataka wasafiri wote waliokuwa Dubai katika wiki mbili zilizopita kuwasiliana haraka na dawati la afya katika wizara ya afya kwa ajili ya kuwafuatilia zaidi. Ameongeza kuwa jumla ya wasafiri 2,661 wametambuliwa kama kuwa hatarini ambao aidha wamejiweka karantini wenyewe ama wamewekwa karantini katika maeneo maalum.

    Wakati huohuo, watoa huduma za kifedha nchini Uganda wanapunguza gharama zao ili kuwawezesha wateja wao kukabiliana na janga la mlipuko wa virusi vya Corona ambalo linatarajiwa kuathiri vibaya uchumi wa nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na Benki ya Stanbic imesema Benki hiyo inashirikiana na Shirikisho la Mabenki la Uganda kuwasaidia wateja wao katika wakati huu wa shida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako