• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Wuhan kuondoa vikwazo vya kutoka nje kuanzia tarehe 8 mwezi Aprili

    (GMT+08:00) 2020-03-24 17:39:55

    Serikali ya mkoa wa Hubei leo imetangaza kuwa, mji wa Wuhan ulioathiriwa vibaya na maambukizi ya virusi vya Corona utaondoa vikwazo vya kutoka nje kuanzia tarehe 8 mwezi ujao baada ya mji huo kufungwa kwa zaidi ya miezi miwili.

    Taarifa iliyotolewa na makao makuu ya uongozi wa udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona ya mkoa wa Hubei imesema, watu waliopo mjini Wuhan wataruhusiwa kuondoka mjini humo na mkoa wa Hubei wakiwa na kibali cha kijani cha afya, kinachomaanisha kuwa hawakuwasiliana mtu mwenye maambukizi ama kushukiwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

    Mji wa Wuhan utachukua hatua tofauti za kurudisha shughuli za biashara kwa kuzingatia tishio la afya kwenye maeneo tofauti ili kukabiliana na athari za kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako