• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: sekta za utalii, uchukuzi, na kilimo zitakuwa na wakati mgumu

  (GMT+08:00) 2020-03-24 18:36:28

  Serikali imesema sekta za utalii, uchukuzi, kilimo zitakuwa na wakati mgumu zaidi waklati huu, wa janga la Coronavirus ambayo kufikia sasa watu 16 wamepatika na virusi hivyo vya corona nchini Kenya.

  Akiongea baada ya mkutano na Shirikisho la Waajiri wa Kenya (FKE) na Vyama vya Wafanyikazi, waziri Kazi Simon Chelugui amesema kuwa serikali inaandaa safu ya maoni yenye lengo la kulinda ajira na biashara.

  Mkutano wa tatu wa wadau katika sekta ya kazi ulikuja masaa kadhaa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza mipango ya mkutano wa kisekta na kutangaza hatua za kukabiliana na biashara zinazoweza kujikuta zikiwa katika shida ya kifedha baada ya janga hili ambalo linaonekana kuenea haraka.

  Jumuiya ya Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) imethibitisha kuwa janga la coronavirus inauweza kusababisha upotezaji wa ajira zaidi ya milioni 25 ulimwenguni pote mwishoni mwa mwaka huu.

  Uchumi wa dunia unatarajiwa kupata hasara ya karibu dola trilioni 3.4.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako