• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watatu kutoka Nigeria walazwa hospitali baada ya kumeza vidonge vingi vya Chloroquine

    (GMT+08:00) 2020-03-24 20:12:50

    Watu watatu kutoka Nigeria wamelazwa hospitali baada ya kumeza vidonge vingi vya Chloroquine, dawa ya kutibu ugonjwa wa malaria kwa imani kuwa inaweza kutibu virusi vya corona.

    Jana, Shirika la Utangazji la Marekani CNN liliripoti kuwa, wiki iliyopita, rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Ikulu kuwa matokeo ya majaribio ya awali ya dawa ya Chloroquine katika kutibu virusi vya Corona yameonekana kufanikiwa, na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani imeidhinisha matumizi ya Chloroquine katika kutibu ugonjwa huo. Lakini Mamlaka hiyo baadaye ilitoa taarifa ikisema tathmini kuhusu ufanisi wa Chloroquine bado inaendelea kufanyiwa, na bado haijatoa idhini ya kutumika kwa dawa hiyo.

    Hata hivyo baadhi ya sehemu nchini Nigeria zimeshuhudia ongezeko la manunuzi ya dawa hiyo na kusababisha bei yake kupanda, na hata baadhi ya maduku ya dawa yanafanya kauli ya rais Trump kama matangazo na kuhamasisha watu kununua Chloroquine.

    Meneja wa mradi wa operesheni za dharura wa Ofisi ya Shirika la Afya Duniani barani Afrika Michel Yao amesema, dawa takriban 20 ikiwemo Chloroquine zinafanyiwa majaribio ya kitabibu na nchi mbalimbali kwa ajili ya kuangalia ufanisi wa kutibu virusi vya Corona, na sasa ni mapema kuipendekeza dawa yoyote. Amesema, WHO haijapata ushahidi kamili wa kupendekeza dawa yoyote.

    Wakati huohuo, wanandoa wenye umri wa miaka 60 jimboni Arizona Marekani nao pia walitumia Chloroquine kukinga virusi vya Corona, ambapo mume alifariki dunia na mke yupo katika hali mahututi na anatibiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako