• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KARATE: Tanzania yaalikwa Michuano wa Karate ya Japan

  (GMT+08:00) 2020-03-25 08:56:37

  Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Karate imepata mwaliko wa kwenda kushiriki katika mashindano ya Dunia ya Karate Japani Oktoba mwaka huu. Mashindano hayo ya Karate ya Dunia huwa yanafanyika kila baada ya miaka mitatu na mwaka huu Tanzania imepata nafasi ya kipekee kwa kutoa jaji wa michuano hiyo (Sensei) Jerome Mhagama. Haya ni mashindano ya 15 ya Dunia tangu kuanzishwa kwake na Tanzania imewahi kushirikiki mara mbili katika mashindano hayo. Kwa mara ya kwanza mwaka 2011 mashindano hayo yaliyofanyika Thailand, Tanzania Ilipeleka mchezaji mmoja tu ambaye ni Mhagama na alifika katika hatua ya 16 Bora. Mwaka 2014 Katika mashindano yaliyofanyika Japan, Tanzania Ilishiriki katika mashindano hayo kwa kupeleka Jaji, ambaye pia alikuwa ni Mhagama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako