• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yakusanya fedha ili kutokomeza kifua kikuu

    (GMT+08:00) 2020-03-25 09:54:53

    Waziri wa afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe amesema serikali ya Kenya inapanga kukusanya fedha za ndani kwa ajili ya kutibu na kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu.

    Kwenye taarifa iliyotolewa katika Siku ya Kifua Kikuu Duniani, Bw. Kagwe amesema fedha hizo zitatolewa na wadau husika, wenzi wa ushirikiano na wanaochangia fedha, na zitatumika katika kuzuia na kutibu ugonjwa wa kifua kikuu, ili kuhakikisha wananchi wote wanaelewa na kutilia maanani zaidi ugonjwa huo mpaka mwaka 2025.

    Ameongeza kuwa kwa sasa wagonjwa 688 walioambukizwa na kifua kikuu wanapewa matibabu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako