• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michango ya China yafika Hispania wakati nchi hiyo inajitahidi kupambana na virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-25 10:28:28

  Michango ya vifaa vya usafi iliyotolewa na serikali ya China, kampuni na jamii ya wachina nchini Hispania, inaanza kufika nchini humo wakati Hispania inapambana na mlipuko mkubwa wa virusi vya Corona, ambao mpaka sasa watu wapatao elfu 40 wameambukizwa na kusababisha vifo vya watu 2,696.

  Hispania kwa sasa iko katika nafasi ya pili kwa idadi ya maambukizi barani Ulaya, ikiifuata Italia.

  Kwa mujibu wa ripoti ya Ubalozi wa China mjini Madrid, shehena ya vifaa kwa ajili ya mapambano dhidi ya virusi ilifika kwenye uwanja wa ndege wa Adolfo Suarez-Barajas mjini Madrid Machi 22. Vifaa hivyo ni pamoja na mask elfu 50, nguo za kujikinga elfu 10, miwani ya kujikinga elfu 10, jozi elfu 10 za glavu za kidaktari na vitendanishi 834 vya kupima virusi vya Corona kwa ajili ya watu elfu 20. Vifaa hivyo vimepokewa na serikali ya Serikali na vinatarajiwa kusambazwa kwa haraka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako