• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wapokea vitendanishi vya kupima COVID-19 kutoka China

  (GMT+08:00) 2020-03-25 10:28:47

  Serikali ya China imechangia zaidi ya vitendanishi 10,000 vya kupima ugonjwa wa COVID-19 kwa Umoja wa Afrika (AU), ikiwa ni sehemu ya pili ya msaada wa China kwa ajili ya kuimarisha juhudi za Kituo cha udhibiti wa magonjwa Afrika (Afrika CDC) kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

  Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya jamii Amira Elfadil amesifu uungaji mkono wa China kwa mapambano dhidi ya virusi vya Corona barani Afrika.

  Baada ya sherehe ya kukabidhiana vifaa hivyo, kamishna huyo na balozi wa China kwenye Umoja wa Afrika na Kamati ya uchumi wa Afrika wa Umoja wa Mataifa (UNECA) Bw. Liu Yuxi wamefanya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya serikali ya China na Umoja wa Afrika kwenye mapambano dhidi ya COVID-19.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako