• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ikulu na baraza la seneta nchini Marekani zafikia makubaliano kuhusu COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-25 18:50:27

    Ikulu ya Marekani na baraza la seneta la bunge la nchi hiyo leo zimefikia makubaliano ya kutoa mpango wenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 2 kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na athari mbaya ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa uchumi wa nchi hiyo.

    Mpango huo ulitolewa baada ya majadiliano magumu ya siku nne kuanzia Alhamis iliyopita baada ya kiongozi wa baraza hilo Bw. Mitch McConnell kuwasilisha pendekezo la chama cha Republican katika juhudi za kupunguza changamoto za kiuchumi kutokana na maabukizi ya virusi vya Corona.

    Baraza la seneta na baraza la wawakilishi la bunge la Marekani yanatakiwa kupitisha muswada huo kabla ya kuupeleka kwa rais Donald Trump wa Marekani kusainiwa ili kuwa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako