• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Awamu ya pili ya vifaa vya kupima virusi vya Corona vilivyotolewa na China kwa Afrika yakabidhiwa kwa Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-03-25 20:10:42

    Awamu ya pili ya vifaa vya kupima virusi vya Corona vilivyotolewa na serikali ya China kwa nchi za Afrika imekabidhiwa kwa Umoja wa Afrika katika hafla iliyohudhuriwa na balozi wa China kwenye Umoja wa Afrika Bw. Liu Yuxi na kamishna wa Umoja huo anayeshughulikia masuala ya kijamii Bi. Amira El Fadil.

    Balozi Liu ameushukuru Umoja wa Afrika na nchi za Afrika kwa kuunga mkono juhudi za China za kupambana na virusi vya Corona wakati hali ya maambukizi ilikuwa mbaya, na sasa China inazisaidia nchi za Afrika kukabiliana na virusi hivyo kwa kutoa vifaa vya matibabu na kueleza uzoefu wake kwa njia ya video. Amesema hii imeonesha urafiki mkubwa kati ya China na Afrika haswa katika kukabiliana na taabu kwa pamoja. Ameongeza kuwa China itaendelea kuongeza nguvu ya kuzisaidia nchi za Afrika katika mapambano hayo.

    Kwa upande wake, Bibi Amira ameshukuru serikali ya China na asasi za kiraia za China kwa kutoa vifaa vya matibabu, na kusema tangu virusi vya Corona vilipuke, serikali ya China imechukua hatua madhubuti, na kufanikiwa kudhibiti maambukizi, jambo lililoipatia dunia muda wa kujiandaa na vita hivyo na uzoefu mwingi. Amesisitiza kuwa China imetoa taarifa kwa wakati kwa jamii ya kimataifa kuhusu maendeleo mapya ya maambukizi na hatua za kukabiliana nayo. Amesema Afrika inapenda kuendelea kuongeza ushirikiano na China katika kupambana na virusi na kujifunza uzoefu wake mzuri

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako