• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Barcelona yautema usajili wa Pierre-Emerick Aubameyang

    (GMT+08:00) 2020-03-26 09:41:26

    Barcelona imeachana na wazo la kumsajili nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang katika usajili wa mwisho wa msimu huu. Badala yake Barcelona inataka kujikita katika usajili wa nyota wa Inter Milan, Lautaro Martinez. Wakati klabu hiyo ikimpa kisogo mshambuliaji huyo, Inter Milan inaweza kumpoteza Martinez. Matumaini ya Aubameyang ambaye ni nahodha wa Gabon, kuongeza mkataba Arsenal ni hatua inayozipa nafasi klabu za Ulaya kumnyakua. Barcelona inaonekana kuvutiwa na ubora wa Martinez kuliko Aubameyang ambaye amecheza kwa kiwango bora msimu huu akiwa Arsenal. Mkataba wa mshambuliaji huyo unamalizika mwakani majira ya joto na Manchester United inahusishwa na mpango wa kumsajili. Licha ya Aubameyang mwenye miaka 30 kusisitiza ana furaha, lakini klabu yake hadi sasa haijafanya mazungumzo naye ya kuongeza mkataba. Arsenal ilitoa Pauni milioni 56 kuipatia Borussia Dortmund ili kupata saini ya nyota huyo wa Gabon Januari, 2018. Aubameyang amefunga mabao 20 katika mashindano yote msimu 2019-2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako