• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaitaka Marekani iache kuiba siri na kufanya udukuzi katika mtandao wa Internet

  (GMT+08:00) 2020-03-26 20:31:59

  Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya China Ren Guoqiang amesema, katika suala la usalama wa mtandao wa internet, Marekani inaongoza kwa kufanya udukuzi duniani, na China inaitaka Marekani iache mara moja kitendo hicho dhidi ya China.

  Shirika la Habari la Reuters limesema, uchunguzi uliofanywa na kampuni ya Qihoo 360 umeonesha kuwa "APT-C-39" inayomilikiwa na Shirika la Upelelezi la Marekani CIA imefanya mashambulizi na kujipenyeza kwenye mtandao wa internet dhidi ya taasisi mbalimbali za China kwa miaka 11. Akizungumzia hili leo hapa Beijing, msemaji huyo amesema inafahamika duniani kuwa Marekani imekuwa ikiiba siri, kufanya upelelezi na mashambulizi dhidi ya serikali, kampuni na watu binafsi wa nchi nyingine kwenye mtandao wa internet. Ameongeza kuwa China inaitaka Marekani ichangie ujenzi wa mtandao wa internet ulio na amani, usalama, uwazi na ushirikiano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako