• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawaziri wa Afya wa nchi za Afrika Mashariki waahirisha mkutano wa ana kwa ana kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-26 20:53:55

  Mawaziri wa Afya kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameahirisha mkutano wa ana kwa ana mpaka virusi vya Corona vitakapodhibitiwa.

  Katika taarifa yao ya pamoja iliyotolewa jijini Nairobi, Kenya, mawaziri hao wamesema kuanzia sasa mikutano yote itafanyika kwa njia ya video, kupitia mtandao wa internet na Skype. Mawaziri hao wamzitaka taasisi za kikanda kutumia teknolojia ya kisasa kama kufanya mkutano kwa njia ya video kama sehemu ya mkakati wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

  Mawaziri hao kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Sudan Kusini na Uganda wamezielekeza nchi hizo kutekeleza kwa asilimia 100 upimaji katika forodha kwa kutumia mfumo wa njia nyingi ili kuepusha mapungufu yoyote.

  Pia wamezitaka serikali za nchi hizo kuunga mkono kampuni za ndani ili kuinua uzalishaji wa bidhaa zinazotumika katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona ikiwemo visafisha mikono, vifaa vya tiba, na sabuni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako