• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri wa mambo ya nje wa China aeleza mafanikio ya mkutano maalumu wa kilele wa G20

    (GMT+08:00) 2020-03-27 10:28:50

    Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria mkutano maalumu wa kilele wa kundi la nchi 20 (G20) kuhusu kukabiliana na virusi vya Corona. Baada ya mkutano huo uliofanywa kwa njia ya video, naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Ma Zhaoxu alieleza mafanikio yaliyopatikana kwenye mkutano huo.

    Bw. Ma amesema, kwenye mkutano huo rais Xi Jinping ametoa hotuba kuhusu "Kushirikiana kupambana na virusi na kutatua changamoto kwa pamoja", na kutoa mapendekezo muhimu kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kimataifa dhidi ya virusi vya Corona na kutuliza uchumi wa dunia, kwenye msingi wa uzoefu wa China katika mapambano dhidi ya virusi hivyo, ambayo yamechukua nafasi muhimu ya uongozi.

    Bw. Ma amesema, pande mbalimbali za mkutano huo zimeahidi kuchukua hatua zote ili kupambana na virusi vya Corona, kulinda maisha ya watu, kuhimiza uchumi, pia zimekubaliana kupashana habari husika kwa wakati, kuhakikisha utoaji wa vifaa vya matibabu, na kutoa msaada kwa nchi zinazoendelea na kukamilisha mfumo wa afya ya umma duniani. Vilevile zimeahidi kudumisha utulivu wa uchumi na soko la fedha duniani, na kupunguza athari za mlipuko wa virusi vya Corona kwa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako