• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za kiarabu zanufaika na uzoefu wa China katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-27 10:30:02

    Maofisa na wataalamu wa China na nchi zaidi ya 10 za Asia Magharibi na Afrika Kaskazini ikiwa ni pamoja na Palestina, Lebanon, Sudan na Kuwait jana walifanya mkutano kwa njia ya video kuhusu kupambana na virusi vya Corona.

    Wataalamu walioshiriki kwenye mkutano huo wamesema uzoefu wa China katika kupambana na virusi vya Corona umeweka mfano mzuri kwa nchi za kiarabu.

    Maofisa wa afya wa Ukanda wa Gaza na Palestina wamesema wamejadiliana mpango wa kukabiliana na virusi na kuwatibu wagonjwa, na kufuata hatua kama za China tangu ilipotokea ripoti ya mtu wa kwanza kuambukizwa nchini humo, pia imechukua hatua ya karantini kama ilivyofanya China. Mtaalamu wa hospitali ya Ibn Al-Nafees ya Syria Bw. Mazen Qusaibati amesema wanahitaji msaada wa China katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Mjumbe wa Shirika la Afya Duniani nchini Lebanon Bw. Iman Shankiti amesema uzoefu wa China unasaidia kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona kote duniani. Maofisa wa Sudan na Kuwait pia wameisifu China kwa kuzipatia mfano wa kuigwa kwenye mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako