• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba muhimu kuhusu kupambana na COVID-19 katika Mkutano maalumu wa viongozi wa G20

    (GMT+08:00) 2020-03-27 10:57:06

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa kwa kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona, serikali na watu wa China siku zote zinatoa kipaumbele katika usalama wa maisha na afya ya watu, na kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa, hivi sasa hali ya kudhibiti virusi hivyo nchini China imeonesha mwelekeo mzuri, huku utaratibu wa uzalishaji mali na maisha ukirejeshwa.

    Rais Xi amesema hayo kwenye hotuba aliyotoa kuhusu kushirikiana kupambana na virusi na kutatua changamoto kwa pamoja, kwenye mkutano maalumu wa viongozi wa kundi la G20 uliofanywa kwa njia ya video juu ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Rais Xi amesema hivi sasa ugonjwa huo unaenea duniani, China ikiwa na wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, inapenda kutoa misaada kwa nchi nyingine kadiri iwezavyo, ili kuchangia utulivu wa uchumi duniani.

    Pande zote zilizoshiriki kwenye mkutano huo zimekubailiana kuwa, ili kukabiliana na msukosuko huo unaowakabili binadamu wote, hakuna nchi yoyote inayoweza kuepuka, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua madhubuti, ili kulinda usalama wa maisha na afya ya umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako