• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Riadha za Dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20 zaahirishwa kutokana na maambukizi ya corona

    (GMT+08:00) 2020-03-27 12:12:39

    Riadha za Dunia kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20 zilizokuwa zifanyike jijini Nairobi kati ya Julai 7-12, zimeahirishwa kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), maamuzi hayo yalifikiwa baada ya mashauriano ya kina na wahusika mbalimbali, pamoja na mashirikisho ya wanachama yaliyokuwa yashiriki mashindano. Waziri wa Michezo Amina Mohammed, alipongeza hatua ya IAAF na serikali ya Japan ambayo pia iliahirisha Olimpiki za Tokyo 2020. Riadha nyinginezo za dunia ambazo tayari zimeahirishwa ni ile ya Indoor Championships mjini Nanjing, China; Nusu Marathon ya Dunia mjini Gdynia, Poland na Matembezi yaliyokuwa yaandaliwe mjini Minsk, Belarus. Nchini Kenya, mamia ya wanariadha tayari wamesimamisha mazoezi katika kambi 20 za mazoezi zilizoko Kaunti ya Nandi kutokana na virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako