• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Man City yasikitishwa na Liverpool kwa kutotaka kuona wakicheza UEFA Champions League

    (GMT+08:00) 2020-03-27 12:14:56

    Klabu ya Man City ya Uingereza imeripotiwa kusikitishwa baada ya kudaiwa kufahamu kuwa Liverpool ni miongoni mwa klabu za EPL ambazo hazitaki kuona wao wanacheza UEFA Champions League. Man City waliadhibiwa na FIFA kwa miaka miwili kutoshiriki michuano yoyote ya Ulaya (UEFA Champions League & Europa League) hii ni baada ya kuthibitika kuwa wamevunja sheria ya FFP (Matumizi ya Juu ya Pesa kuliko inachoingiza). Licha ya Man City kukata rufaa katika Mahakama ya Kimichezo (CAS) lakini klabu zilizopo Top 10 Ligi Kuu Uingereza nje ya Man City wameiomba CAS kuwa Man City isiruhusiwe kushiriki michuano ya Ulaya wakati rufaa yake ikiwa inasikilizwa. Hii ni baada ya kuwepo kwa dalili zote kwamba msimu ujao wa UEFA utaanza huku rufaa ya Man City ikiwa bado haijatolewa maamuzi, Man City ameshangazwa kuona Liverpool ni miongoni mwa klabu zilizounga mkono ombi hilo la vilabu vya EPL. Man City wameshangazwa kwa sababu Liverpool wapo juu yao na uwezekano wa kucheza Champions League msimu ujao upo, hivyo walitegemea kuona vilabu vya chini ndio vinalivalia njuga suala hilo sababu ya kutaka nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako