• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: RFEF kuzisaidia klabu zenye hali mbaya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2020-03-27 17:22:31

    Shirikisho la Soka nchini Hispania (RFEF) limetangaza kutoa Euro milioni 500 kwa ajili ya kuzisaidia klabu zilizo kwenye hali ngumu ya kifedha kupambana dhidi ya janga la Corona. Fedha hizo zitatolewa kwa klabu ambazo zitashindwa kupata faida inayotokana na haki ya matangazo ya televisheni katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, na vitatakiwa kurejesha fedha hizo ndani ya miaka mitano ijayo. Shirikisho hilo pia limesema litatoa paundi milioni 3.7 kwa timu zisizoshiriki ligi za kulipwa. Idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya Corona nchini Hispania imepita 3,400.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako