• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Karia, Kaburu waongoza mazishi ya Asha Muhaji

    (GMT+08:00) 2020-03-27 17:23:02

    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Wallace Karia pamoja na viongozi mbalimbali wa soka jana waliungana kumuaga aliyekua Mwandishi mwandamizi na Afisa Habari wa zamani wa Simba Asha Muhaji. Asha Muhaji alifikwa na umauti siku ya Jumatano baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, jijini Dar es Salaam. Enzi za uhai wake, Asha alifanya kazi katika kampuni ya New Habari Ltd, inayochapisha magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania na Rai akiwa mmoja wa waandishi na wahariri waliofanya kazi kwa weledi mkubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako