• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huawei yatoa vifaa vya kufanyia mkutano kwa video nchini Uganda katika kusaidia kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-27 18:40:59

    Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Huawei ya China imetoa msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video nchini Uganda ili kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Kupitia akaunti yake ya Twitter, rais Yoweri Museveni wa Uganda ameipongeza kampuni hiyo, na kusema vifaa hivyo vitawezesha mawasiliano ya haraka kati ya Makao Makuu ya Wizara ya Afya, Hospitali ya Rufaa ya Mulago, na hospitali nyingine nchini humo.

    Naye Waziri wa Afya nchini humo Ruth Aceng amesema vifaa hivyo ni muhimu sana katika kupambana na virusi vya Corona, na kuishukuru Huawei katika kusaidia vita dhidi ya virusi hivyo.

    Kampuni ya Huawei imesema, vifaa hivyo vitawezesha mikutano kwa njia ya simu za kisasa za mkononi na mawasiliano kati ya wafanyakazi katika maeneo kadhaa kama vituo vya afya na Wizara ya Afya. Pia kampuni hiyo imesema, kupitia vifaa hivyo, wataalam wa afya wa Uganda wanaweza kubadilishana uzoefu na wenzao wa China kuhusu mbinu za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako