Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Biashara na Ustawi wa Kiviwanda Betty Maina alisema kando na kuokoa maisha ya Wakenya hatua hiyo inalenga kulinda viwanda vya kutengeneza nguo vya humu nchini. Marufuku hii ambayo inaathiri wafanyabiashara wengi wa mitumba nchini Kenya, imejiri wakati ambapo waziri wa Afya Mutahi Kagwe kutangaza kuwa idadi ya watu walioambukizwa nchini humo imepanda hadi 31.
Hii ni baada ya watu wengine watatu kugunduliwa kuwa na virusi hivyo kufikia Alhamisi.
Bw Kagwe amesema visa vya maambukizi vimeathiri zaidi kaunti za Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |