• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waomba mfumo uuzaji korosho ghafi uangaliwe

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:01:53

    Mamlaka ya kiwanda cha kubangua na kuchakata korosho cha Yalin Cashewnut Company Limited kilichoko mkoani Mtwara Tanzania kimeiomba serikali ya nchi hiyo kuweka utaratibu mwingine wa uuzaji wa korosho ghafi, ili kuwawezesha wenye viwanda vya kuchakata korosho nchini humo kupata mali ghafi hiyo kirahisi na kwa bei nafuu.

    Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Sulaiman Millanzi, amesema utaratibu uliopo kwa sasa, unawataka wenye viwanda kununua mali ghafi hiyo kupitia minada ambayo inawafanya wakumbane na ushindani mkubwa wa bei kutoka kwa wanunuzi ambao wanasafirisha korosho ghafi kwenda nje ya nchi.

    Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, imeweka utaratibu mpya wa uuzaji na ununuzi wa mazao ya biashara hususan korosho, ikiwataka wanunuzi wote wa mazao hayo kununua kupitia minada inayofanyika kwenye vyama vya ushirika nchini humo lengo likiwa ni kuhakikisha wakulima wananufaika na bei ya mazao yao.

    Mwaka wa fedha 2018/19, serikali ilipanga bei elekezi ya Sh. 3,300 kwa kilo ya korosho na kuwataka wanunuzi wote kununua korosho za daraja la kwanza kwa bei hiyo, uamuzi ambao ulisababisha wanunuzi wengi kugomea kununua zao hilo kwa kisingizio kwamba bei elekezi ilikuwa kubwa na wasingeweza kupata faida wakati wa kuuza.

    Kufuatia mgomo huo, serikali ilinunua korosho zote zaidi za tani 200,000 kutoka kwa wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako