• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za Kenya kusaidia wakulima Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:02:09
    Kampuni mbili za kimataifa nchini Kenya, zitaanza kuwafuta machozi wakulima wa mazao ya mboga na nafaka wa vijiji vya pembezoni kati ya Wilaya ya Moshi na Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikilalamikia kukosa soko la uhakika la mazao.

    Meneja Miradi wa Taasisi ya Kiserikali ya Rikolto Kain Mvanda inayowasaidia wakulima nchini Tanzania kupata masoko ya uhakika, amesema kampuni hizo zipo tayari kununua tani 180 kwa mwezi.

    Mvanda alitangaza neema hiyo kwa wakulima hao, baada ya kukutana na kuafikiana na menejimenti za Kampuni ya Fresh Mart na Molly Flowers ya Kenya ambayo yananunua mazao ya mboga kwa wakulima.

    Kwa mujibu wa Mvanda, hivi sasa kampuni hizo tayari zimeanza mchakato wa kuonana na wakulima na taasisi zinazowasaidia wakulima, na kuingia mikataba ya ununuzi wa mazao hayo.

    Aidha, alisema wakulima wa Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na tatizo kubwa la masoko ya mazao ya mboga wanayolima na hivyo kuwasababishia wengine kukata tamaa ya kuendelea na kilimo hicho.

    Alisisitiza kuwa ujio wa kampuni hizo za kununua mazao ya wakulima, utasaidia kutatua kero ya muda mrefu ya mazao kukosa masoko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako