• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Uingereza athibitishwa kuwa na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:18:59

    Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imesema leo kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Borris Johnson amethibitishwa kuwa na virusi vya Corona.

    Msemaji wa Ofisi hiyo amesema, baada ya kuanza kuonyesha dalili hapo jana, Bw. Johnson alipimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Amesema Waziri Mkuu huyo amejitenga ofisini kwake, na anaendelea kuongoza serikali katika kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo.

    Zaidi ya watu 11,600 wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Uingereza, na zaidi ya watu 570 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako