• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa kipaumbele kuzuia maambukizi ya virusi vya corona kutoka nje

    (GMT+08:00) 2020-03-27 21:21:29

    China imeweka kipaumbele kwa kazi za kuzuia virusi vya Corona kuingia nchini humo kutoka nje na wimbi jipya la maambukizi kuibuka ndani ya nchi.

    Hayo yamesemwa kwenye mkutano wa ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC leo hapa Beijing ulioendeshwa na rais Xi Jinping wa China kuhusu kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona na kutathmini hali ya uchumi.

    Mkutano huo pia umesisitiza kuwa, mbali na kufanya vizuri kazi za kukabiliana na virusi vya corona, ni lazima kuongeza kasi ya kurejesha utaratibu wa shughuli za uzalishaji na maisha, kupunguza kabisa athari mbaya zinazotokana na maambukizi ya virusi, kufanya juhudi za kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi yaliyowekwa kwa mwaka mzima, na kufanikiwa kujenga jamii yenye maisha bora kwa pamoja zote na kuondoa umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako