• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ahadi ya rais Xi kutoa msaada na uzoefu wake juu ya COVID-19 yapongezwa duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-28 19:31:25

    Ahadi ya rais Xi Jinping wa China ya kuendelea kutoa mbinu bora kwa wengine na kusaidia nchi zinazoathirika na COVID-19 imepongezwa na waangalizi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

    Kwenye mkutano wa viongozi wa Kundi la nchi 20 uliofanyika Alhamis, rais Xi alisema China iko tayari kutoa mbinu bora kwa wengine, kufanya utafiti wa pamoja na kuendeleza dawa na chanjo, na kutoa usaidizi kadiri iwezavyo kwa nchi zinazokumbwa na mlipuko unaoendelea kukua.

    Akipongeza mchango uliotolewa na China mhariri mkuu wa jarida la Nouvelle Solidarite la Ufaransa na mtaalamu wa Taasisi ya Schiller France Bi. Christine Bierre amesema hatua nzuri za China za kupambana na virusi vya Corona, pamoja na juhudi Zake za kusaidia nchi nyingine kwa kutuma wataalamu wa afya na vifaa vya kujilinda, au kupanga mkutano kwa njia ya video kwa ajili ya wataalamu wa afya, ni nzuri. Naye Mhadhiri wa mambo ya kiuchumi wa Chuo Kikuu cha Nairobi Gerishon Ikiara amesema China imeeleza uzoefu wake, kutoa vifaa vya kimatibabu na kiufundi pamoja na wataalamu wa afya kwenye nchi nyingi ili kuzisadia kupambana na virusi vya Corona.

    Kwa upande wa Mwanahabari wa Saudia ambaye pia ni mtafiti juu ya China Abdulaziz Alshabaanai pamoja na Mwenyekiti wa zamani wa Shirikisho la Habari la Oman Awad Baqwer wamesema China imefanya kazi nzuri ya kudhibiti mlipuko nyumbani na uzoefu huu unafaa kuigwa, na kwamba China iko mstari wa mbele katika kutoa taarifa za kupambana na COVID-19 kwa Shrika la Afya Duniani WHO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako