• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu laki moja wathibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani  

    (GMT+08:00) 2020-03-28 19:33:21

    Takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani zinaonesha kuwa, hadi kufikia saa 11 na dakika 13 ya tarehe 27 kwa saa za mashariki nchini Marekani, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imefikia 100,717, kati yao watu 1,544 wamefariki, na ongezeko la maambukizi kwa siku limekaribia elfu 20.

    Uwezo wa kupima virusi vya Corona nchini Marekani umeanza kuongezeka. Hata hivyo hadi kufikia tarehe 26, ni jimbo la New York tu lililokuwa limepima watu zaidi ya laki moja, na katika majimbo 36 likiwemo eneo maalumu la Washington, watu waliopimwa ni chini ya elfu 10.

    Wakati huohuo, rais Donald Trump wa Marekani jana alisaini rasmi mswada wa kuhimiza uchumi wa dola trilioni mbili za Kimarekani ili kukabiliana na athari ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako