• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya COVID-19 duniani yafikia laki 5.1

    (GMT+08:00) 2020-03-28 19:45:04

    Ripoti kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya COVID-19 iliyotolewa jana na Shirika la Afya la Dunia WHO ilisema kuwa, hadi kufikia tarehe 27, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya COVID-19 duniani ilifikia 509,164, na idadi ya watu waliokufa ilifikia 23,335.

    Kwenye bara la Ulaya ambalo linakabiliana na hali mbaya zaidi ya maambukizi ya virusi vya COVID-19, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo jana iliongezeka kwa 36,414, na kuifanya idadi ya jumla ya watu wenye maambukizi hayo ifikie 286,697, wakati huohuo, idadi ya watu waliokufa iliongezeka kwa 2,155, na kwa ujumla watu 16,105 wamekufa. Maambukizi ya virusi vya Corona yameathiri nchi na maeneo 201 duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako