• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakosoa vyombo vya habari vya Marekani kwa kutoa barua ya wazi ya kulalamikia serikali ya China

    (GMT+08:00) 2020-03-28 20:10:12

    Maofisa waandamizi wa idara ya habari ya wizara ya mambo ya nje ya China wamekutana na wakuu wa ofisi za vyombo vitatu vya habari vya Marekani vikiwemo New York Times, The Wall Street Journal na The Washington Post mjini Beijing, na kuwakosoa kwa kutoa barua ya wazi ya kulalamikia serikali ya China.

    China iliamua kusimamisha kazi za wanahabari wa vyombo hivyo vitatu ili kulipiza kisasi kitendo cha Marekani kuwanyima haki ya kuripoti wanahabari wa China nchini Marekani.

    Barua hiyo inasema, wakikosekana waandishi wa habari wa Marekani, dunia haitajua hali ya maambukizi ya COVID-19 nchini China. China imesema inapinga kuhusisha uamuzi wake na ripoti kuhusu ugonjwa huo, na pia vyombo hivyo vya Marekani vinafahamu vizuri kama vimetoa habari za ukweli au kupotosha kuhusu juhudi za China kukabiliana na maambukizi ya virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako