• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDO: Rais wa Ngumi za Kulipwa Tanzania kurejea madarakani baada ya miezi sita

    (GMT+08:00) 2020-03-30 08:23:38

    Wakati baadhi ya wadau wa ngumi za kulipwa wakiibua minong'ono kuhusu rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Joe Anea kupumzika kwa miezi sita kiutendaji, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha amesema hakuna kipingamizi kwa Joe kupumzika kipindi hicho kisha kurejea kuendelea na majukumu yake. Hivi karibuni baadhi ya wadau wa ngumi za kulipwa waliibua minong'ono wengine wakitaka kiongozi huyo ajiuzulu nafasi hiyo ili kupisha wengine waendelee, baada ya kuomba kuwa nje kwa matatizo ya kiafya. Msitha amesema Anea atarejea madarakani baada ya miezi sita kupita kama alivyoomba apewe mapumziko katika kipindi hicho kwa masuala ya kiafya. Makamu wa Rais wa TPBRC, Aga Peter alisema kuwa ataendelea kukaimu nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba na kuomba wadau kuendelea kutoa ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako