• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanamgambo waongeza shughuli Afghanistan licha ya juhudi za kuleta amani nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-03-30 10:09:07

    Wanamgambo wa Afghanistan wameongeza shughuli zao ambazo zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 40 katika saa 24 zilizopita, licha ya juhudi zinazoendelea za kuwarejesha kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan kwenye meza ya mazungumzo.

    Chini ya upatanishi wa ujumbe wa Marekani unaoongozwa na mwakilishi maalum wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani anayeshughulikia maridhiano ya Afghanistan Bw. Zalmay Khalilzad, serikali ya Afghanistan imeunda timu ya watu 21 kufanya mazungumzo na kundi la Taliban.

    Msemaji wa Taliban Bw. Zabihullah Mujahid amesema kupitia ukusara wa Twitter kwamba hawataki kufanya mazungumzo na serikali, na badala yake wanataka kuzungumza na timu pana inayoshirikisha vikundi vyote vya Afghanistan, na kuthibitisha kwamba ujumbe wa watu 10 wa Taliban unaoongozwa na Mawlawi Ziaudin hivi karibuni utatembelea Bagram, kuanza mchakato wa kuwaachia uhuru wafungwa katika mpango wa amani wa Marekani na Taliban. Lakini serikali ya Afghanistan bado haikubali kuwaachia wafungwa elfu tano wa Taliban ndani ya siku 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako