• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yahimiza mchango zaidi wa Saudi Arabia katika mapambano dhidi ya nzige

    (GMT+08:00) 2020-03-30 10:09:28

    Iran imeitaka Saudi Arabia ichangie zaidi katika mapambano dhidi ya nzige wa jangwani ambao wanatishia mazao na usalama wa chakula katika kanda ya mashariki ya kati.

    Mkuu wa Shirika la ulinzi wa mimea wa Iran Bw. Mohammad Reza Dargahi amesema nchi za Bahari Nyekundu, haswa Saudi Arabia inapaswa kuisaidia Iran kupambana na nzige mwaka huu ambao wanaweza kuathiri maelfu ya hekta za ardhi ya kilimo , akiongeza kuwa hivi sasa Iran inapambana dhidi ya nzige kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta elfu 45 katika majimbo sita kusini mwa nchi.

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limekadiria kuwa kundi la nzige linaweza kuvamia mkoa wa Kerman, katikati ya Iran na eneo la ardhi oevu la Jazmourian, katika wimbi jipya la uhamiaji wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako