• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping aonesha ishara wazi ya kulinda kwa pamoja utulivu wa mnyororo wa ugavi kwenye mnyororo wa viwanda duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-30 13:04:06

    Tarehe 29 Machi, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara ya ukaguzi kwenye mkoa wa Zhejiang, China. Hii ni mara ya nne kwa rais Xi kufanya ziara ya ukaguzi tangu mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona yalipoanza.

    Kituo cha kwanza - Bandari

    Kituo cha kwanza kwenye ziara ya rais Xi ni eneo la Chuansha lililoko kwenye bandari ya Zhousha, mjini Ningbo, ambapo aliuliza hali kuhusu kurejeshwa kwa uzalishaji mali kwenye bandari hiyo.

    Mwaka jana, Bandari ya Zhoushan ilihudumia tani bilioni 1.12 za mizigo, kiasi ambacho kinashika nafasi ya kwanza duniani kwa miaka 11 mfululizo. Ilihudumia makontena milioni 27.535 na kushika nafasi ya tatu kati ya bandari zote duniani.

    Kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, bandari ya Zhoushan ya mji wa Ningbo ilihudumia tani milioni 163 za mizigo katika miezi miwili ya mwanzo mwaka huu, kiasi ambacho kinachukua zaidi ya asilimia 98 ikilinganishwa na kile cha mwaka jana wakati kama huu; ilihudumia makontena milioni 4.06, kiasi ambacho kilifikia asilimia 90 ikilinganishwa na kile cha mwaka jana wakati kama huu.

    Rais Xi Jinping kufanya ukaguzi wa kazi kwenye bandari hii kubwa zaidi duniani, kumeonesha ishara wazi ya kulinda kwa pamoja utulivu wa mnyororo wa ugavi kwenye migogoro ya viwanda duniani.

    Kituo cha pili-Eneo la uzalishaji wa vielezo vya vipuri vya magari ya hali ya juu

    Kituo cha pili cha ukaguzi wa kazi wa rais Xi Jinping ni Eneo la uzalishaji wa vielelezo vya vipuri vya magari yenye hali ya juu lililoko kwenye mtaa wa Beilun, mjini Ningbo. Hivi sasa eneo hilo linajumuisha zaidi ya viwanda 70, ambalo limechaguliwa kuwa "Kituo cha vielelezo cha viwanda vya Die-casting cha China". Kwenye eneo hilo, rais Xi alikagua kwa makini Kampuni ya vielezo vya mitambo ya Zhenzhi ya Ningbo.

    Hadi kufikia tarehe 26, asilimia ya 90.06 ya uwezo wa uzalishaji mali mkoani Zhejiang ulikuwa umerejeshwa, asilimia 108.58 ya uwezo wa uzalishaji mali wa viwanda vidogo vidogo na vya kati laki 1.1 umerejshwa, asilimia 88.2 ya uwezo wa uzalishaji mali wa wafanyabiashara binafsi umerejeshwa.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, " Katika wakati huo, ni lazima tuwe na mtizamo wa kufikiria kwa pande zote, wa upembuzi, na kutupia macho siku za mbele kuhusu maendeleo ya nchi yetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako