• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuinua uwezo wa safari za anga ili kutuliza minyororo ya ugavi

    (GMT+08:00) 2020-03-30 16:12:17

    Maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China na Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi wamesema, mlipuko wa virusi vya Corona umetoa changamoto kubwa kwa sekta ya safari za ndege za kimataifa za China, na idara husika zimejitahidi kuongeza uwezo wa usafiri wa anga, ili kuhakikisha utulivu wa mnyororo wa ugavi wakati dunia ikikabiliwa na mlipuko wa virusi hivyo.

    Hadi kufikia Machi 26, ndege za mizigo za China zimekamilisha safari 23 za kusafirisha vifaa vya matibabu vyenye uzito wa zaidi ya tani 400, na kutoa mchango katika kutuliza mnyororo wa ugavi wa vifaa vya matibabu duniani.

    Katika siku zijazo, idara husika zitaendeleza ujenzi wa viwanja vya ndege vya uchukuzi wa mizigo, kuhimiza uratibu na ushirikiano kati ya kampuni za ndege na kampuni za uchukuzi wa mizigo, na kujenga vituo vya uchukuzi wa anga, ili kuondoa mapungufu yaliyopo kwenye sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako