• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Victor Wanyama atoa msaada wa chakula kwa wakazi wa Mathare

    (GMT+08:00) 2020-03-30 16:45:59

    Wakazi wa mabanda ya Mathare jijini Nairobi nchini Kenya wana kila sababu ya kutabasamu wakati wakikabiliana na hali ngumu ya uchumi kufuatia mlipuko wa virusi hatari vya corona. Hii ni baada ya nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Victor Wanyama kuonyesha ukarimu wake kwa kutoa msaada wa chakula na vitakasa mikono kwa wakazi hao kama njia ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo. Wanyama alitoa mchango huo siku ya Ijumaa Machi 27, kupitia taasisi yake pamoja na wadau wengine ikiwemo Shirika la Msalaba Mwekundu. Kiungo huyo wa zamani wa Spurs alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe wa kufuata tahadhari huku serikali ikiendelea kupambana na janga hilo. Maoema mwezi huu, Mkenya huyo aliondoka Tottenham kuelekea Canada ambako amejiunga na Montreal Impact.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako