• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klabu zaipinga TFF

    (GMT+08:00) 2020-03-30 16:46:15

    Timu za Ligi Kuu Tanzania Bara zimegomea mfumo mpya unaotarajiwa kuanzishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa kuhakikisha klabu zinatumia kiwango cha fedha halali kulingana na kiasi kitakachokubalika katika uendeshaji kwa msimu. Hivi karibuni, rais wa TFF Wallace Karia alinukuliwa na vyombo vya habari akisema, kwa sasa wanafanya mpango na utaratibu wa kuja na mfumo huo kwa kuanza kukagua timu zinazoshiriki ligi hiyo kama fedha halali wanazoingiza wanatumia ipasavyo. Kwa nyakati tofauti, viongozi wa timu za Simba, Yanga, Azam na Mwadui wamesema mfumo huo sio mwafaka kwa sasa, kwani TFF walitakiwa kufanya mambo ya msingi kama kuandaa mazingira mazuri ya mchezo huo ili klabu ziwe na uwezo wa kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako