• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Riadha ya Dunia kuahirishwa

    (GMT+08:00) 2020-03-30 16:46:34

    Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Riadha (WA) Sebastian Coe amesema, huenda Mashindano ya Dunia ya Riadha 2020 yakasogezwa mbele kwa mwaka mmoja ili kuwezesha Michezo ya Olimpiki kufanyika. Michezo ya Olimpiki Tokyo 2020, ambayo awali ilipangwa kufanyika Japan Julai 24 hadi Agosti 9 mwaka huu, imeahirishwa hadi mwakani kutokana na janga na virusi vya Corona, na mpaka sasa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) haijapanga tarehe mpya ya kufanyika mashindano hayo. Mashindano ya Riadha ya Dunia yalipangwa kufanyika Agosti mwaka ujao, Eugene, Oregon, lakini Coe amesema yanapaswa kusogezwa mbele ili kukwepa kugongana na Olimpiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako