• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Sereikali yazuia kufungwa minada

    (GMT+08:00) 2020-03-30 16:52:31
    Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaani (Tamisemi), wamewaagiza wakurugenzi, watendaji wa mitaa na wakuu wa wilaya zote nchini, kuacha mara moja kufungia minada ya samaki na ile ya ng'ombe kwa kisingizio cha viruso vya korona.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam wikendi iliyopita, naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdalla Ulega, amesema kuwa msimamo wa serikali upo pale pale haujazuia biashara yoyote, ikiwemo minada ya samaki na nyama na walioanza kufungia minada hiyo kuacha mara moja.

    Kauli ya Ulega imekuja kwa kile alichoeleza kuwa tayari kuna taarifa za masoko ya minada kufungwa katika mikoa mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako