• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpaka wa kenya na Tanzania haujafungwa, ila kuna masharti makali.

    (GMT+08:00) 2020-03-30 16:56:32
    Shughuli za biashara kati ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki zimekwama kutokana na kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya korona. Hii ni baada ya mataifa husika kufunga mipaka yake .

    Hata hivyo, Kenya na Tanzania bado hazijafungiana mipaka yake, haswa katika eneo la Namanga. Licha ya hali hii, biashara katika eneo hili la Namanga zimekwama kwa kiwango kikubwa baada ya mataifa haya mawili kuweka masharti makali kwa usafirishaji wa mizigo na watu.

    Uchunguzi unaonyesha kwamba idadi ya malori ya mizigo yanayotoka Kenya kwenda Tanzaniaimepungua mno. Aidha, malori yote ya mizigo yanayotoka Tanzania kuingia Kenya, lazima yasindikizwe na maafisa wa usalama hadi mwisho wa safari na kuhakikisha kwamba yamerejea Tanzania.

    Kenya ina zaidi ya maafisa wa polisi 40 na magari ya polisi katika eneo la Namanga.

    Wiki moja iliyopita, katibu wa Kenya wa maswala ya kijamii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kevit Desai, alisema kwamba kupungua kwa shughuli katika mpaka wa Kenya na Tanzania, kumesababisha hasara ya shilingi bilioni 38 pesa za Kenya ambazo ni sawa na dola milioni 380. Hii ni tangu kuripotiwa kwa mlipuko wa virusi vya korona Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako