• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi za maambukizi ya virusi vya Corona zaendelea kuongezeka duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-30 19:45:51

    Idadi ya jumla ya kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona duniani imefikia 638,146, kati ya hizo, 555,790 zimeripotiwa nje ya China, huku idadi ya vifo vilivyotokana na virusi hivyo duniani ikifikia 30,105 usiku wa jana kwa saa za Ulaya ya Kati.

    Kutokana na Kitivo cha Mifumo ya Sayansi na Uhandisi cha Chuo Kikuu cha John Hopkins, mpaka kufikia jana usiku, Marekani ilikuwa na kesi 142,000 zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, na watu 2,479 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

    Wakati huohuo, Wizara ya Afya nchini Rwanda imeripoti kuwa, kesi 10 mpya zimethibitishwa kuwa na virusi vya Corona, na kufanya idadi ya jumla ya maambukizi nchini humo kufikia 70. Kati ya wagonjwa wapya 10, sita ni wasafiri kutokea Dubai, wawili wanatoka Afrika Kusini, na mmoja ana historia ya kusafiri karika kanda ya Afrika Mashariki.

    Nako nchini Sudan, Wizara ya Afya nchini humo imethibitisha kifo cha pili kinachotokana na virusi vya Corona. Sudan mpaka sasa ina kesi sita zilizothibitishwa kuwa na virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako