• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa wito wa kuzisaidia kampuni ndogo na za kati kurudi kwenye hali ya kawaida

    (GMT+08:00) 2020-03-30 19:52:24

    Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi kwenye mkoa wa Zhejiang, China, akiagiza kuzisaidia kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati kurudi kwenye hali ya kawaida.

    Rais Xi alifanya mkutano na wawakilishi wa kampuni ndogo na za kati katika kituo cha huduma na usimamizi wa Eneo la kutengeneza vipuri vya magari vyenye ubora wa juu lililoko kwenye mtaa wa Beilun, mjini Ningbo.

    Katika mkutano huo, Rais Xi alisema, kampuni na sekta mbalimbali zimeathiriwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imetathmini hali hiyo, hasa ikitilia maanani kampuni ndogo na za kati, na kutunga sera ili kuyasaidia. Pia itarekebisha sera hizo kutokana na mabadiliko ya hali, ili kuyasaidia makampuni hayo kutoathiriwa vibaya na yaweze kupata maendeleo mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako