• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jamii ya kimataifa yapaswa kuangalia hali halisi ya China katika kufanya ushirikiano kupambana na mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-30 20:01:39

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema, anatarajia pande husika zitaangalia kwa usahihi hali halisi ya China katika kufanya ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, na kuchukua hatua zaidi zitakazosaidia kushinda mapambano hayo.

    Bibi Hua amesema, watu wa China hawatasahau misaada kutoka jumuiya ya kimataifa walipokuwa wakipitia wakati mgumu, pia China itatoa misaada kadri inavyoweza kusaidia nchi mbalimbali. Amesisitiza kuwa, katika mapambano hayo, kusaidia wengine ni kujisaidia mwenyewe.

    Bibi Hua pia amesema, kampuni za China zimefanya kazi ya ziada kutengeneza vifaa vya matibabu kwa ajili ya kutoa misaada kwa nchi nyingine, na jitihada hizo za China zinapaswa kuheshimiwa badala ya kulaumiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako