• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya Olimpiki Tokyo kufanyika Julai 23 hadi Agosti 8 mwaka 2021

    (GMT+08:00) 2020-03-30 20:39:52

    Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesema, Michezo ya Olimpiki ya Tokyo itafanyika kuanzia Julai 23 hadi Agosti 8 mwaka 2021, karibu mwaka mmoja baada ya ratiba ya awali.

    Mashindano hayo yalipangwa kuanza Julai 24 mwaka huu, lakini yaliahirishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona. Tarehe mpya imetangazwa baada ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Kamati ya Kimataifa ya Mashindano ya Walemavu, Kamati ya maandalizi ya Tokyo 2020, Serikali ya Mji wa Tokyo na serikali ya Japan kufikia makubaliano mapema jumatatu.

    Michezo ya walemavu itafanyika kuanzia Agosti 24 mpaka Septemba 5 mwaka ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako