• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Hisa za Juventus zapanda thamani baada ya kukata mishahara wachezaji

    (GMT+08:00) 2020-03-31 08:32:39

    Hisa za Juventus jana zilipanda thamani baada ya uamuzi wa klabu hiyo kukata mishahara wachezaji katika kukabiliana na athari za mlipuko wa virusi vya corona. Mabingwa hao wa soka wa Serie A walitangaza Jumamosi iliyopita kuwa wamekata mishahara ya wachezaji wao kuanzia Machi hadi Juni baada ya michezo yote nchini Italia kusimamishwa. Hisa za klabu hiyo zilipanda kwa asilimia 7.94 jana asubuhi katika Soko la Hisa la Milan ambalo limeathiriwa sana na virusi vya corona. Wachezaji wa Juventus wenye mishahara mikubwa ni pamoja na Christian Ronaldo, ambaye ameshatwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mara tano na kiungo wa Wales, Aaron Ramsey, ambaye alijiunga na klabu hiyo akitokea Arsenal katika uhamisho ambao haukuwa na ada. Taarifa ya klabu inasema ilikubaliwa kuwa athari za kiuchumi na kifedha kwa mwaka 2019/20 zinafikia dola milioni 100.5. Juventus, ambayo ilikuwa juu ya Lazio kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi moja kabla ya msimu kusimamishwa Machi 9, iliongeza kuwa kama msimu utamaliziwa mwaka huu, wachezaji wanaweza kulipwa ziada katika miezi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako